Taarifa iliyotolewa mapema leo December 11 2016 asubuhi na msemaji wa idara ya taifa ya mambo ya dharura nchini Kenya Pius Masai amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba magari zaidi ya 11 yameteketezwa kwa moto katika barabara ya Nairobi-Naivasha.
Maafisa kutoka wizara ya usafirishaji wakiongozwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Irungu Nyakera
wamewasili katika eneo la tukio na Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watu
wengi wamejeruhiwa na miongoni mwao ni watu waliokuwa wakirejea nyumbani
kutoka harusini subukia.
Katibu mkuu Irungu amesema kuwa kwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa
ajali hiyo imetokana na dereva kutokufahamu vizuri barabara hiyo
kutokana na kwamba lori hilo la mafuta ni la nchini Uganda
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment