Kwanini unavutiwa na sauti ya watangazaji fulani na
nyengine unazichukia? Vipi unasikika ukiwa hewani? Cathy Loughran,
mhariri wa chuo cha BBC anazungumza na wajuzi na wakufunzi ambao
wamefunza vizazi kadha
Maoni yaliyokusanywa na Radio Times hivi karibuni kuhusu sauti zinazovutia yameonesha wanaoongoza ni Eddie Mair wa Radio 4 na Kirsty Young, wote wawili wanatoka Scotland.
Matokeo yamenifanya niulize walimu wawili wenye uzoefu, kuhusu sauti zinazovutia kwa sasa, na kwa jumla, sifa ya sauti zinazosikika uzuri kwenye redio.
Mchezaji filamu wa zamani, Kate Lee, amekuwa akifunza watangazaji kwa miaka 25, pamoja na BBC, ITN na Channel 4 News. Elspeth Morrison ni mtayarishaji wa zamani wa vipindi vya TV, ambaye anashughulika na kushirikiana na mashirika yote makubwa ya utangazaji, na anawafunza wachezaji sinema matamshi ya makabila tofauti.
Hapa wanaonesha ufundi wao na kukushauri namna ya kusikilizana vema kwenye maiki.
Kate Lee
“Jee inashangaza kuwa sauti mbili zinazopendwa kabisa ni kutoka Scotland? Nafikiri tunajua siku zote kuwa watu wanapenda sauti za Scotland. Waskochi wakizungumza ni kama wanaimba kidogo, ambayo inavutia.
Nafikiri ni shida zaidi kwa wanawake. ‘Nani mwenye sauti nzuri?’ mara nyingi inamaanisha ‘nani mwenye sauti nene?’. Wanawake wengi wanahisi wazungumze sauti ya chini kuvutia. Ukizungumza hivyo wakati wote, utaiumiza sauti yako.
Ushauri wangu muhimu kwa watangazaji
-
Huna sauti , unatumia sauti. Inavoelekea unaweza kuisarifu sana sauti yako kushinda unavyofikiri, kwa hivyo usiogope.
-
Utangazaji unahitaji nguvu kushinda watu wanavyofikiri. Sipendi kutoa
ushauri unaosikia mara nyingi ‘waza kuwa unazungumza na mtu fulani’;
kama manake ukizungumza na mtu mmoja huna haja ya kujitahidi sana, kwa
sababu mtu mmoja tayari uko naye.
-
Jipatie joto kidogo. Koo iwe imetulia vya kutosha. Ni vema kuimba hali midomo imefungwa na kuvuta pumzi kwa wingi”
“Sauti nzuri” inategemea anayeisikiliza. Sauti nyingi zinazoongoza ni nzuri, lakini baadhi nahisi, hazitumiwi kwa mapana yake, na zinasikika doro kidogo.
Kuna shinikizo kwa watangazaji wa kike, washushe sauti yao, ambayo inaweza kufanya sauti kusikika kama ya ashiki. Wakati mwengine hiyo haifai kwa kusoma taarifa ya habari.
Pengine mimi nashughulika zaidi na hisia za vizazi tofauti. Maoni yaliyokusanywa na Radio Times.com ya watu wanaosoma tovuti yao, tofauti na wasomaji wa gazeti, walipendekeza majina 10 tofauti, na kwengine yalifanana.
Watu waliokuwa chini ya umri wa miaka 30, wanaonesha hawavutiwi na ‘sauti nzuri’ kama wasikilizaji waliowazidi umri.
Niliwahi kufanya majaribio na wanafunzi wa michezo ya kuigiza wa umri wa miaka 18, nikatumia sauti laini ya Charlotte Green – namba mbili kati ya zinazopendwa – akisoma habari katika Radio 4, na msomaji habari wa redio inayotoa matangazo, mwenye kisauti chembamba. Ingawa wanafunzi kwa jumla walipenda sauti nene ya Charlotte, walihisi walipata habari zaidi kutoka kwa mtangazaji wa sauti ya juu na ambaye sauti yake ilipanda kidogo mwisho wa sentensi.
Mimi naamini watangazaji wazuri wanazaliwa na kipaji. Lakini wakipata msaada watu wengi wanaweza kujifunza kutia mkazo kwenye vipi pamoja na kipi wanachosema.
Shauri muhimu kwa watangazaji wa redio
-
Usipige kelele kwenye maiki. Fikiria kama unazungumza kwa sauti yako ya kawaida na mtu aliye kando nawe.
-
Vuta pumzi kama kawaida – ukiwa unahitaji kupitia mdomoni – kuepuka
kusikilizana kama una wasiwasi. Unaweza kuweka alama katika maandishi
yako, ambapo unaweza kusita kidogo ili uweze kupumua.”
0 comments:
Post a Comment