Baada ya Ligi Kuu soka Tanzania bara round ya pili kukaribia kuanza December 17 2016, Yanga waliamua kufanya maboresho ya kikosi chao na kuleta kocha mpya George Lwandamina kutoka Zambia na kumbadilishia majukumu aliyekuwa kocha wao Hans van Pluijm kuwa mkurugenzi wa ufundi.
Leo December 10 2016 kocha Lwandamina amekaribishwa kwa kipigo akiwa anaiongoza Yanga katika mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi ya timu ya JKU ya Zanzibar, Yanga wakiwa uwanja wa Uhuru, huku mchezo huo ukiaminika ungekuwa mwepesi kwao, wamekubali kipigo cha goli 2-0 magoli yakifungwa na Emanuel Martin.
Kocha George Lwandamina anaonekana kutumia mchezo huo kujua uwezo wa wachezaji wake mmoja mmojai, hiyo inatokana na kuamua kuchezesha vikosi viwili ikiwa kipindi cha kwanza alichezesha timu nyingine na cha pili timu nyingine, Lwandaminaambaye anasema kuwa hajawahi kufeli ameanza kwa kipigo akiwa na Yanga.
0 comments:
Post a Comment