January 23 2017 timu ya taifa ya Algeria iliingia uwanjani kucheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B AFCON 2017 dhidi ya Senegal katika uwanja wa Franceville, Algeria walikuwa wanaingia kucheza mchezo huo wakihitaji ushindi lakini kufuzu kwao kulitegemea matokeo ya mchezo mwingine.
Algeria waliingia uwanjani kucheza na Senegal wakiwa wanahitaji ushindi huku wakiiombea mabaya Tunisia ambayo ilikuwa inacheza na Zimbabwe, kwa bahati mbaya Algeria walilazimishwa sare ya 2-2 na Senegal lakini hata kama wangepata ushindi, ushindi wa 4-2 wa Tunisia dhidi ya Zimbabwe ungewaondoa mashindanoni.
Magoli ya Algeria yalifungwa na staa wao anayeichezea Leicester City ya England Slim Slimani dakika ya 10 na dakika ya 52 lakini magoli ya Papa Diop dakika ya 44 na Musa Sow dakika ya 53 yaliufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2 na kuifanya Algeria iage michuano hiyo bila kupata ushindi wowote
0 comments:
Post a Comment