www.kenethngamoga.blogspot.com

Aliyeokolewa kutoka Boko Haram asema anamkosa baba wa mtoto

Msichana mmoja raia wa Nigeria ambaye aliokolewa kutoka mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, amesema anamkosa sana mpiganaji wa kundi hilo ambaye ni baba wa mtoto wake
Rais Buhari alikutana na Amina Ali baada ya kuokolewaImage copyrightREUTERS
Image captionRais Buhari alikutana na Amina Ali baada ya kuokolewa
Msichana mmoja raia wa Nigeria ambaye aliokolewa kutoka mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, amesema anamkosa sana mpiganaji wa kundi hilo ambaye ni baba wa mtoto wake.
Amina Ali ni mmoja wa wasichana mia mbili wa shule ya Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliyopita.
Amesema kile anachotaka sasa ni kwenda nyumbani.
Madaktari wa kijeshi wamchunguza mtoto baada ya kuokolewaImage copyrightNIGERIA MILITARY
Image captionMadaktari wa kijeshi wamchunguza mtoto baada ya kuokolewa
Yeye pamoja na mtoto wake wamekuwa wakizuiliwa katika mjini Abuja, katika kile serikali inasema ni mpango wa kumwezesha kutengamana na watu tena.
Amina Ali alipatikana katika msitu mmoja mapema mwaka huu akiwa na mtoto wake na mtu mmoja ambaye alisema ni mumuwe ambaye ni mpiganaji wa kundi hilo la Boko Haram
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment