Baada ya taarifa hizo kuenea viongozi wa kanda wa Yanga walikaa na kuamua kufanya mkutano wa dharura leo August 16 makao makuu ya klabu yao, moja kati ya viongozi wa matawi ya Yanga mkoa wa Dar es Salaam anayeiwakilisha kanda ya Temeke Robert Liungu ametaja maazimio waliyofikia kutoka katika mkutano wa dharura.
1- Wanachama wa Yanga wanatambua kuwa Manji bado ni mwenyekiti wao kwa mujibu wa katiba yao.
2- Wanachama wamemuomba mdhamini Mzee Katunda amtoe mzee Akilimali anayedaiwa kumpinga Manji atolewe katika nafasi ya katibu wa wazee wa Yanga.
3- Wanachama wanaiomba kamati ya utendaji ya Yanga imuite mzee Akilimali imuhoji na kumsimamisha uanachama kwa madai kuwa yeye ni Simba.
4- Wanachama wa matawi yote wanaendelea kumtambua Yusuph Manji kama mwenyekiti wao
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment