Aidha vyama vingine vya siasa vimeonyesha dhamira ya kupinga kile ambacho kitasemwa na wapinzani wao. Vyanzo hivyo vya habari vimebainisha kwamba upo uwezekano mkubwa wa kutokea vurugu baina ya makundi mawili ya kisiasa.
kupitia taarifa hiyo Jeshi la Polisi nchini limepiga marufuku maandamano na mikutano ya hadhara kuanzia June 07 2016 hadi hapo hali ya usalama itakapotengemaa.
Jeshi la Polisi limewataka wanasiasa kuacha mara moja kuwashinikiza wananchi kutotii sheria za nchi. Jeshi la Polisi halitasita kumchukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote au chama chochote cha siasa kitakachokaidi agizo hili.
Aidha taarifa hiyo imewataka wananchi kuwa makini na wanasiasa wenye lengo la kutaka kuvuruga amani ya nchi hii na badala yake linawasihi waendelee kushirikiana katika kujenga umoja wa nchi hii.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment