www.kenethngamoga.blogspot.com

MAMA ASIMULIA BANGI ILIVYOMPATIA AFYA MWANAE ANAYEUGUA SARATANI

Mwanamke Callie Blackwell kutoka nchini Uingereza, aeleza jinsi ambavyo bangi ilivyomsaidia mwanaye aliyeugua saratani kwa muda mrefu kupata ahueni.

Mwanamke huyo alieleza kuwa kijana wao alikuwa na ugonjwa wa saratani ambao ulimfanya kuwa mdhaifu sana na kumtesa.
Kijana Deryn Blackwell alisumbuka sana. Mnamo mwaka 2010 akiwa na miaka 10 aligundulika kuwa ana saratani ya damu.
Miezi 18 baadaye, aliambiwa kuwa ana saratani nyingine ambayo ni nadra sana. Uvimbe ambao umewahi kuwapata watu 50 tu duniani na ni watu watano tu wanaougua ugonjwa huo kwa sasa duniani. Lakini hakuna mtu aliyewahi kutambulika kuwa na saratani za aina mbili kwa wakati mmoja, jambo lililomfanya Deryn kuwa wa kipekee. Mvulana mmoja kati ya watu bilioni 70.
Amekuwa na maumivu makali na kila mara alitakiwa kutumia dawa za kupunguza maumivu.
Mwaka 2013 baada ya kukaa hospitali kwa miaka minne kwa ajili ya matibabu, madaktari waliona kuwa kilichobakia ni yeye kutumia dawa za kupunguza maumivu huku akisurubia wakati wake wa kufa.

Japokuwa madaktari walionyesha kukata tamaa na hali ya mwanangu, lakini mimi sikukata tamaa. Niliendelea kutafuta mtandaoni ni kwa namna gai ningeweza kumuokoa mwanangu kutoka katika maumivu anayoyapata.
Ndipo nilipopata aina fulani ya “bangi” iliyokuwa ikitumiwa kutuliza maumivu. Haikuwa inapatikana Uingereza, kwa hiyo ilibidi tuiagize japo ilikuwa ni haramu.
Sikuwahi kuona faida yoyote ya kuvuta bangi na niliichukia bangi kila mara. Lakini mimi na mume wangu hatukuwa na namna.
Tulihitaji bangi kwa ajili ya kumtengenezea Deryn dawa hiyo ya kupunguza maumivu aliyokuwa akiyapata.
Mume wangu, Simon alipanga kukutana na mtu ambaye angempatia bangi hiyo. Alielewa vyema kuwa kukamatwa akiwa na bangi atahukumiwa kwenda jela miaka mitano, na kuhukumiwa miaka 14 ukipatiakana ukiwa unamuuzia mtu mwingine.

Nimewahi kuona taarifa kwenye runinga, za wazazi walionyang’anywa watoto wao pale walipogundulika kuwa wanawapa dawa za kulevya kama bangi. Mume wangu hakuogopa, alitaka kama ni kulaumiw alaumiwe yeye, ilimradi tu mwanetu apone.
Simon aliporudi hospitali tuliitengeneza dawa ile kwa kutumia bangi. Deryn alipovuta ule moshi wa bangi na kuutoa nje, baada ya dakika 10 alianza kusema kuwa anasikia maumivu yakipungua mwilini mwake.
Siku moja niliwaza, kama kiwango kidogo tu cha bangi kilimsaidia mwanangu kwa kiasi hicho, je itakuwaje nikimpa zaidi? haitomfanya apone kabisa?

Maswali hayo yalimfanya mama yake Deryn kuamua kuongeza kiwango cha bangi ili ampe mwanae. deryn alipoimeza ile bangi alikaa kwa muda wa nusu saa kisha akasema hahisi maumivu mwilini mwake.
“Nahisi utulivu, naelewa kila kitu, najisikia nina amani. hii ni nzuri mama” alisema Deryn
Image result for deryn blackwell
Nesi aliingia katika wodi ile na kutaka kumchoma deryn sindano ya dawa ya kupunguza maumivu. Lakini deryn aliikataa akisema kuwa hasikii maumivu yoyote.

Miezi illizidi kupita huku nikimpa deryn kiwango kidogo cha bangi na hali yake ilizidi kuwa nzuri. Hata baadhi ya vidonda vilivyokuwa katika vidole vyake vilianza kupona.
Hata Daktari alipokuja alishangazwa na hali yake. alipokuja hospitali, deryn alipewa siku tatu tu za kuishi na baada ya hapo angekufa, lakini sasa ni miezi imepita.
“Huu ni muujiza. watu wengi walikuwa wakimuombea Deryn ili apone. Hakika huu ni muujiza .“ Alisema mwanamke huyo.

“Sikuwahi kuwaambia madaktari wala mtu mwingine kuwa nilikuwa nikimpa mwanangu bangi. Ni kwa vile niliogopa kama mamlaka ingejua na kunichukulia hatua.”
“Lakini nimeamua kuisimulia hadithi hii ili madaktari na wataalamu wengine waendelee kufanya uchunguzi na huenda wakapata suluhu ya kuwasaidia wengine.”
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment