Picha ya kwanza kabisa ya mapacha wasichana walioshikana na mabao walitenganishwa katika upasuaji wa kihistoria Kenya na Afrika imetolewa.
Wasichana hao wawili wenye umri wa miaka 2 waliozaliwa mnamo 2014 walikuwa wameshikana katika eneo la nyonga na upande wa chini wa uti wa mgongo.
Ilichukua juhudi za kundi madaktari 60 kuwatenganisha wasichana hao katika masaa 23, katika shughuli ya kwanza kabisa ya upasuaji wa aina hiyo kuwahi kufanyika Kenya mnamo Jumanne, Novemba 1 saa 6 asubuhi hadi Jumatano mnamo Novemba 2 saa 5 asubuhi.
Kundi hilo lilijumuisha wapasuaji wa watoto, wapasuaji wa ubongo, wataalam wa kurekebisha maungo na wataalam wengineo pamoja na kundi la wauguzi.
Madaktari wanonea fahari upasuaji huo muhali, ambao ni wa kwanza kabisa kufanyika nchini Kenya na Bara la Afrika.
Shughuli yote ya upasuaji iligharimu KSh 150 million.
“Angalau sasa naweza nikatabasamu. “Namshukuru Mungu na kundi lililokuwa katika chumba cha upasuaji lililonihakikishia kuwa Mungu ana ushukani. Nilitulia nilipoona wote wana imani thabiti katika Miungu na wakati shughuli ya upasuaji ilipoisha wasichana wangu walitenganishwa, nilifurahi sana,” alisema Caroline Mukiri, mamake wasichana hao katika mahojiano nya hapo awali.
Alidhihirisha furaha yake baada ya wasichana hao kuanza kupumua pekee yao baada ya kuondolewa kwenye mashine.
Majuma mawili baadaye, leo hii mnamo Jumanne Novemba 15, picha ya kwanza kabisa ya wasichana hao waliotenganishwa ilitolewa.Wasichana hao kwa sasa wanapata afueni katika Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.
Wakenya walipongeza kundi hilo la wataalam pamoja na hospitali hiyo kwa kufanikisha shughuli hiyo muhali na kuiweka Kenya na vituo vyake vya matibabu kwenye historia.
0 comments:
Post a Comment