Vichwa vya habari jana na leo ni kuhusu Tanzania kuishinda Angola kwenye michuano ya soka la wenye umri chini ya miaka 17 huko Gabon na nyingine ni kuhusu Mchezaji wa Serengeti Boys baada ya hiyo mechi kudaiwa kupimwa na CAF kama alitumia dawa za kuongeza nguvu.
Abdul Hamis Selemani aliyeifungia Serengeti Boys goli la pili ambae pia alitajwa kuwa Mchezaji bora wa mechi ndio aliripotiwa kuwa alichukuliwa kwenda kupimwa kwa kushukiwa kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha kwenye hiyo game vs Angola licha ya kutoka majeruhi.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas ambaye alikuwa Libreville Airport kujiandaa na safari ya kwenda Port Gentil na kusema “ Niwatoe shaka Watanzania kwamba kuchukuliwa vipimo kujua kama Mchezaji katumia dawa za kusisimua misuli au la ni utaratibu wa kawaida “
‘ Daktari husika wa mchezo anaesimamia ni lazima kila mwisho wa mchezo achukue vijana wawili wa kila timu akawapime ili ajiridhishe kwenye kuandika ripoti yake kama ambavyo Mwamuzi na Wasimamizi wengine wanavyoandika ripoti zao’
0 comments:
Post a Comment