Mwanamke aliyefahamika kwa jina Jessica Hawayu katika Kaunti ya Tana River nchini Kenya amenusurika kifo baada ya kumeza pete ya uchumba iliyokuwa imewekwa ndani ya pilau kwa ajili ya mchumba wake kumfanyia ‘sapraizi’.
Jessica aliokolewa na baba yake mzazi baada ya kupewa huduma ya kwanza kisha kuitema pete hiyo. Sherehe ya uchumba ya Jessica ilipangwa na familia yake kwa ushirikiano na mchumba wake Johanna Charo.
Tovuti ya Tuko ya nchini Kenya ilieleza kwamba sherehe hiyo ya kutoa mahari iliiingia dosari baada ya Jessica kumeza pete iliyokuwa imefichwa kwenye sinia la pilau, katika hali isiyo ya kawaida akajikuta ameichota kwenye tonge kisha kula na muda mfupi alikabwa kooni
Hata hivyo, mchumba wake Johannah Charo alieleza kuwa kusudio lake ilikuwa kumfanyia ‘surprise' mchumba wake ili asijue ni jambo gani lilikuwa limewakutanisha kusherehekea siku hiyo.
Awali, Charo kwa kushirikiana na mama yake Jessica, walipanga jinsi angemfurahisha mchumba wake na ndipo wakakubaliana kuiweka pete ndani ya sahani ya pilau.
"Pilau ndio chakula ambacho Jessica anakipenda na kwa hiyo alipoelezwa kusaidia kukiandaa, alijitolea kwani alijuaa anamuandalia baba yao," alisema Melanie Hawayu ambaye ni dada yake Jessica.
Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa baba mzazi alipinga pete kuwekwa ndani ya pilau kwani alihofia kuwa ingeleta madhara.
"Baba hakukubaliana na mpango wetu lakini kwa sababu tulikosa mbinu nyingine, tuliamua kuendeleza mpango wetu wa awali tuliokuwa nao," amesema Melanie.
Amesema wakati hayo yote yakipangwa nyumbani kwao Jessica mpenzi wake Charo pamoja na marafiki zake walikuwa wanasubiri ishara kutoka kwa wakwe zake watarajiwa kuwa kila kitu kimekwenda sawa.
Sherehe hiyo ilitaka kugeuka msiba punde baada ya Jessica kumeza pete hiyo ya uchumba.
Hata hivyo, baba yake mzazi alimpigapiga mgongoni na kuifanya pete hiyo kutoka.
Kutokana na tukio hiyo Jessica alizimia kutokana na mshtuko kisha alipelekwa kupelekwa hospitalini baada ya kupata fahamu.
0 comments:
Post a Comment