Afya ni muhimu kwa kila binadamu, ndiyo maana wataalamu wa afya wamekuwa wakitoa ushauri mara kwa mara kwamba unapojisikia hali yako siyo nzuri,
jitahidi kwenda hospitali kupata matibabu sahihi yatakayokufanya upone.
Jenga afya yako kwa kutambua umuhimu wa Afya ya binadamu, imekuwa ikiwashauri wananchi kula vyakula vitakavyowajenga, kuimarisha na kuufanya mwili uwe na afya njema kutokana na vyakula hivyo kuwa na vitamini vya kutosha.
Safu hiiinaangazia muda sahihiwa kula chakula (cha asubuhi, mchana na usiku kabla ya kwenda kulala).
Chakula kinatakiwa kinatakiwa kiliwe kwa muda sahihi ambao utakifanya kifanye kazi ya kujimeng’enya tumboni, badala ya kula mfululizo bila kupumzika.
ni vyema binadamu afuate utaratibu unaopaswa wakati unapotaka kula kati ya mlo mmoja na mwingine ili kulipa tumbo nafasi ya kupokea chakula kingine.
Unapoamka asubuhi, jitahidi kunywa maji nusu lita kabla ya kupiga mswaki na baada ya kufanya hivyo kaa muda wa dakika 30 na baada hapo pata kula kifungua kinywa chako.
Jitahidi kifungua kinywa chako kiwe muda wa saa tatu na nusu na usile vyakula ambavyo vitakufanya upate usingizi asubuhi hiyo.
Unaweza kunywa chai kwa andazi moja, baada ya kufanya hivyo kaa muda wa dakika 30 kisha kula matunda yako kwa sababu ulipoamka asubuhi ulikunywa maji, hivyo hauna haja ya kula matunda muda huo.
Kifungua kinywa hicho kitafanya kazi vizuri kwa sababu ulitanguliza maji na baada ya dakika 30 ulikula matunda, ambayo yatakuongezea nguvu ya kufanya mmeng’enyo mzuri wa chakula tumboni.
Baada ya muda wa saa nne tangu ulipopata kifungua kinywa, pata chakula cha mchana na jitahidi usile chakula kingi ambacho kitakufanya uvimbiwe.
Kabla ya kula chakula cha mchana unaweza kuanza na matunda kwa ajili ya kuliandaa tumbo kwa kupokea chakula, na baada ya kula kaa muda wa nusu saa ndipo sasa unywe maji.
Ni vizuri ukajenga utamaduni wa kula chakula kwa kuanza na matunda na baadaye chakula, ila kwa asubuhi, jitahidi kunywa maji kwanza kabla ya kifungua kinywa.
Muda sahihi wa kula chakula cha mchana hadi saa saba na fahamu kuwa hata maofisini kuna muda ambao umepangwa kwa ajili ya kupata chakula cha mchana.
Utumie muda huo kuhakikisha kwamba unalitimizia tumbo lako mahitaji yake ili kujiepusha na magonjwa vikiwemo vidonda vya tumbo kutokana na kukaa muda mrefu bla kupata chakula.
Hata hivyo, inashauriwa kuwa baada ya kula chakula usipende kulakula hovyo bila mpangilio kwani vitu vidogo unavyokula ndivyo vinavyokufanya unenepe .
Pia, muda mzuri zaidi wa kula mlo wa uiku ni kuanzia saa 12 jioni hadi saaa 2 usiku. Jitahidi kutokula chakula kingi wakati wa usiku.
Baada ya kula pumzika kwa saa chache ili chakula kiweze kukaa vizuri na kumeng’enywa tumboni. jitahidi sana kuepuka vyakula vya wanga wakati wa usiku.
Unaweza kula matunda na mboga mboaga ambazo zimechemshwa bila kuwekwa viungo na kunywa maji ambayo yatasaidia katika mmeng’enyo.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment