www.kenethngamoga.blogspot.com

Kabila: Sitowania urais tena

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amewahakikishia raia wake kwamba ataheshimu katiba ya nchi na kwamba hatawania urais katika Uchaguzi mkuu ujao

Akilihutubia bunge la taifa, Kabila ameomba kuwepo amani na utulivu.
"Kwa wale ambao wanaingilia kati maisha yangu ya siasa kila siku, nina sema asante lakini wafahamu ya kwamba Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongomani" Alisema Kabila.
Kabila ni mmoja wa marais wenye umri mdogo barani AfrikaImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionKabila ni mmoja wa marais wenye umri mdogo barani Afrika
Jana waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.
Hatua hii ni ya kutuliza msukosuko wa kisiasa nchini DRC baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment