www.kenethngamoga.blogspot.com

Kutana na jamaa aliye na wake 97 na watoto zaidi ya 190 (picha)

Jina la Alhaji Pa Bello Abubakar Masaba ni maarufu sana nchini Nigeria. Usiumize kichwa ukijaribu kukumbuka uvumbuzi wa kisayanzi alioufanya mzee huyo wa miaka 80.
Hata hivyo, alilofanya Masaba sio jambo la kawaida..
Masaba ana wake 97 na watoto zaidi ya 190.
Alhaji Pa Bello Abubakar Masaba ana wake 97 na watoto zaidi ya 190. Picha: Naij.com
Alhaji Pa Bello Abubakar Masaba ana wake 97 na watoto zaidi ya 190. Picha: Naij.com
Kulingana na mtandao wa naij.com, Masaba alishitakiwa mwaka 2008 kwa kuvunja sharia ya Kiislamu inayoweka wazi mwanaume anaweza kuoa hadi wanawake wanne.
Hata hivyo kesi hiyo haikufua dafu baada ya wake 57 kushuhudia mahakamani kuwa walikubali kuolewa naye kwa hiari.
Kutana na jamaa aliye na wake 97 na watoto zaidi ya 190 (picha)
Baadhi ya ukoo wa Alhaji Pa Bello Abubakar Masaba.
Masaba ni mwalimu wa dini ya kiislamu.
Katika mahojiano na gazeti la kigeni, Masaba aliutaja uwezo wake kuwatosheleza kimapenzi wake hao 97 kama kipawa kutoka kwa Mungu.
“ Mwenyezi Mungu kwa hekima yake amenipa nguvu ya kuwatosheleza. Wangekuwa tayari wamenitoroka iwapo singekuwa nikiwatosheleza”
Nchini Kenya, marehemu Akuku Danger alijizolea sifa kwa kuoa zaidi ya wake 100 na kuzaa watoto karibu 200.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment