www.kenethngamoga.blogspot.com

Simba yakwaa kisiki kwa URA, yalazimishwa sare

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo wamekwaa kisiki katika kampeni yao ya kutafuta ushindi katika mechi za maandalizi za kujifua kujiandaa na ligi kuu Tanzania Bara, msimu wa 2016/17 kwa kulazimishwa sare na URA ya Uganda.
Baadhi ya wachezaji wa Simba katika dimba la Taifa Dar es salaam
Simba iliyosheheni wachezaji wengi wapya, hii leo imejikuta ikilazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Taifa Dar es salaam.
Ikicheza mbele ya mamia ya mashabiki wake ambao katika siku za karibuni wameonekana kuanza kuwa na imani na timu yao, imejikuta ikitangulia kufungwa bao katika dakika ya 19 kupitia kwa Elkanah baada ya shambulio la URA lililomlazimu beki wa Simba Mwanjare kuokoa kwa kichwa cha nyuma mpira ambao ulitua miguuni kwa mshambuliaji huyo wa URA, na kumalizia nyavuni.
Baada ya bao hilo Simba ambayo ilianza mechi kwa kucheza mchezo wa kujiamini na pasi nyingi zilizokuwa hazielekei katika lango la wapinzani, walibadilika ghafla na kuanza kusukuma mashambulizi kwa nguvu, hali iliyopelekea kupata bao la kusawazisha kupitia kwa nahodha Jonas Mkude aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mohamed Hussein Shabalala.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu hizo zilikuwa sare ya bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu zote kuoneshana ufundi na kiwango, lakini hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibaki 1-1.
Katika mchezo wa leo, imeshuhudiwa nahodha mstaafu wa Simba Musa Hassan Mgosi akivua rasmi kitambaa cha unahodha, na kuwaaga mashabiki pamoja na wachezaji wenzake.
Mgosi aliingia dimbani katika kipindi cha Kwanza na kucheza kwa takriban dakika 3, kisha kuvua kitambaa kumkabidhi Jonas Mkude na kutoka nje kwa ajili ya kuwaaga mashabiki ka kuzunguka uwanja mzima.
Huo ni mchezo wa pili wa kimataifa wa Simba baada ya ule iliyocheza katika siku ya Simba (Simba Day) na kuichapa FC Leopard maba 4-0.

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment