Siku 29 pekee kuelekea oktoba 25 mwaka huu, sauti bado ni ile ile kila kona ya nchi akiwa mjini hai ambapo alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya lunongai, shirimatunda, machame na hai mjini Edward Lowasa amesema atahakikisha anaongoza nchi kwa misingi ya haki na usawa huku akiahidi kutumia vema ilani ya ukawa kuhakikisha anapambana na rushwa kwani kwa muda mrefu imekuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchi huku wachache wakinufaika na rasilimali za nchi.
Huku akionekana kujiamini kushinda katika uchaguzi ujao, Freeman Mbowe anayewania nafasi ya ubunge katika jimbo hilo la hai amewataka wanahai na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanafanya mabadiliko kwani ndio njia pekee ya kujikwamua na umasikini uliokithiri hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.
Fredrick Sumaye waziri mkuu mstaafu akihutubia maelfu wakazi wa jimbo la hai amesema ni wakati muafaka wa kukiondosha chama cha CCM madarakani kwani kimeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na kufanya nchi kuendelea kuwa masikini.
0 comments:
Post a Comment