Msimu wa joto huuoooo waja na joto likipamba moto ni mtafutano kweli kweli! Feni hunguruma mchana kutwa, usiku kucha na kwa wale waishio uzunguni ni mwendo wa kiyoyozi tuu…
Msimu wa joto huuoooo waja na Daslam joto likipamba moto ni mtafutano kweli kweli! Feni hunguruma mchana kutwa, usiku kucha na kwa wale waishio uzunguni ni mwendo wa kiyoyozi tuu…
Sasa jua linapokuwa la utosi na kusababisha joto kali wengi hupendelea kuvalia kandambili ili miguu ipate hewa; lakini yawezekana wewe unaevalia kandambili hizo kuna mambo kadha wa kadha ambayo huyafahamu.
Sio vibaya kuvalia kandambili lakini wataalamu wa magonjwa ya miguu wanatoa tahadhari kwamba kuvaa viatu vya kanda mbili mara kwa mara kunaweza kuiharibu miguu yako.
Kwanza, kanda mbili zilizoko kati ya vidole vyako zinasugua ngozi na misuli yako na kusababisha ugonjwa wa misuli ya miguu.
Pili, ukivaa viatu vya aina hiyo mara kwa mara, kutasababisha utembee kwa hatua mfupi zaidi kuliko kawaida na hali hiyo itaharibu viungo vyako.
Na tatu, viatu vya kanda mbili haviwezi ‘kufix’ nyayo zako vizuri na katika hali hiyo, ukitembea kwa muda mrefu, inawezekana kuharibu umbo wa miguu yako na hata viungo vyao.
Ungana na mimi kupitia
Facebook ,
Twitter na
Instagram Pia subscribe
Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
0 comments:
Post a Comment