Wakati Watanzania wengi macho na masikio yetu tukiwa tumeyaelekeza kwenye utoaji wa tuzo za MTVMama ambazo zimetolewa Afrika Kusini lakini usiku huo huo wa Oct 22 kuamkia Oct 23 nchini Marekani kulikua pia kukitolewa tuzo ambazo Watanzania wenzetu pia walishiriki.
Tuzo ambazo zilitolewa marekani zinajulikana kama African Entertainment Awards Usa 2016 (AEA) kitu kizuri na kikubwa ni kwamba Watanzania wenzetu wameshinda pia kwenye tuzo hizo kwenye baadhi ya vipengele.
Kipengele cha Msanii bora anaechipukia kashinda Harmonize,Kipengele cha wimbo bora wa kushirikiana/kushirikishwa umeshinda wimbo wa Zigo wa AY,Kipengele cha DJ Bora niDj D Ommy na msanii bora wa kiume kashinda Diamond Platnumz.
Tuzo aliyoshinda Harmonize alikua anashindana na Tekno Miles,Ziza Bafana,Ayo Jay,Missy Bk,Jay Oliver,Den G,Togar Howard na Ziza Bafana.Tuzo aliyoshinda AY wimbo bora wa kushirikiana alikua akishinda na Nagharamia ya Christian Bella na Alikiba,Woju ya Kiss Daniel akiwa kamshirikisha Davido na Tiwa Savage,Pimpina ya Obrafour akiwa kamshrikisha Bisa Kdei,Porque te amo ya To Semedo akiwa kamshirikisha Boss Ac na wimbo wa Nagode wa Yemi Alade akiwa kamshirikisha Selebobo.
Tuzo aliyoshinda Dj D Ommy alikua akishinda na Dj Tunez,Dj Van,Dj Mensah,Dj Brazao,Dj BossMan na Dj Jimmy Jatt,tuzo ya msanii bora wa kiume aliyoshinda Diamondkipengele hicho alikua na Eddy Kenzo,Wizkid,Mc Galaxy,Nelson freitas,Coreon Du naMaster jake.
Baada ya tuzo kukamilika Rayvanny aliamua kutuonyesha tuzo hizo kupitia video hii fupi.
0 comments:
Post a Comment