www.kenethngamoga.blogspot.com

Real Madrid na Atletico Madrid wamefungiwa kufanya usajili hadi January 2018

Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo September 8 2016 limetangaza rasmi kukataa rufaa za vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid vya Hispania, FIFA wamekataa rufaa ya Real na Atletico iliyokuwa inafungia kufanya usajili katika madirisha mawili
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA leo September 8 2016 limetangaza rasmi kukataa rufaa za vilabu vya Real Madrid na Atletico Madrid vya Hispania, FIFA wamekataa rufaa ya Real na Atletico iliyokuwa inafungia kufanya usajili katika madirisha mawili.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Real Madrid na Atletico walifungiwa na kamati ya nidhamu ya FIFA mwezi January kutofanya usajili kwa madirisha mawili kutokana na kukiuka kanuni za FIFA za usajili, kwa kufanya usajili wa wachezaji wa chini ya miaka 18 wasio raia wa Hispania.
Adhabu hiyo wataanza kuitumikia kuanzia sasa kwani awali ilishindika kutokana na vilabu hivyo kukata rufaa, hivyo Real Madrid na Atletico Madrid hawatoruhusiwa kufanya usajili hadi January 2018, adhabu hiyo pia inaambatana na faini ambapo Real Madridwatatakiwa kulipa pound 249,00 na Atletico pound 622,000, vilabu hivyo vinaweza kufanya usajili lakini havitaruhusiwa kuwatumia wachezaji hadi 2018.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment