Ripoti hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Dkt. Hellen Kijo-Bisimba kwenye mazungumzo maalum na East Africa Television ilipotaka kujua kundi gani katika jamii ya watanzania linaongoza kwa kuwafanyia watoto vitendo vya ukatili na nini suluhisho la kukomesha tatizo hilo kwa kutumia sheria za kimataifa zakuwalinda watoto.
Dkt. Kijo-Bisimba amesema kutokana na wahusika wa ukatili huo kuwa ni wanafamilia inasababisha kuwa na ugumu wa kufanya maamuzi kwa kuwa kama ni mzazi amefanya anajilinda kwa kuyamaliza kifamilia na wengine wanafanya vitendo hivyo kwa kulipiza visasi hali ambayo ameipinga vikali mkurugenzi huyo.
Dkt. Kijo-Bisimba amesema sheria ya mtoto iko wazi kuzuia ukatili kwa watoto usitokee kwa kutumia mamlaka ya vyombo vya usalama na ustawi wa jamii kwa kuwakamata wahusika na kuwawajibisha kwasababu kuna baadhi ya adhabu zinakiuka haki za watoto.
Ameiasa serikali kupeleka watumishi wa ustawi wa jamii maeneo ambayo hayana watumishi hao ili kunusuru kizazi cha sasa na baadaye sambamba na kuzuia vitendo hivyo visiendelee kutokea nchini ili jamii iishi kwa amani na upendo.
Kwa upande wa mtaalam wa Saikolojia na mambo ya kifamilia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam Dkt.Chriss Mauki amesema ukatili wa kijinsia unachangiwa na umaskini wa kukosa fikra sahihi za kufanya maamuzi yaliyo sahihi hivyo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha inawalinda watoto wote bila ubaguzi.
0 comments:
Post a Comment