Instagram imezindua
nembo mpya katika hatua ya kutaka kujiboresha na kutoonekana kuwa programu ya
picha pekee Nembo
hiyo imetengezwa kuimarisha ujumbe unaotumwa.
Nembo hiyo inaonyesha kamera ya kawaida na rangi za upinde wa mvua. Zaidi ya picha milioni 80 na video husambazwa kila siku katika mtandao wa Instagram, mtandao huo una takriban wateja milioni 400 na uliipiku Twitter mwaka 2014.
Viongozi
wa mtandao wa Instagram waliiambia Newbeat, “Wakati Instagram ilipokuwa inaanza
ilikuwa na eneo la kukarabati na kusambaza picha. Miaka mitano baadaye likawa
ni eneo linalopendwa na jamii kubwa ulimwenguni ambapo watu husambaza picha na
video.”
Watumiaji
pia watagundua kwamba eneo la bluu katika nembo ya mtandao huo limeanza
kubadilika na kuwa jeupe. Mtindo huo mpya una lengo la kuimarisha picha na
video zinazotumwa bila kubadilisha unavyoingia katika mtandao huo. Ubunifu wa
nembo hiyo mpya ulianza mwaka mmoja uliopita.
Aidha
walitaka kutengeza nembo ambayo ingewakilisha mahitaji ya awali ya sasa na ya
siku za baadaye.
0 comments:
Post a Comment