Kampuni ya kubashiri ya SportPesa tayari ni wadhamini rasmi wa Simba, hatua hiyo imefikiwa baada ya kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 4.9.
Hii inaiondoa Simba kwenye hasara ya msimu mzima. Kwani ilikuwa ikicheza bila ya kuwa na mdhamini baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kutotaka kuendelea.
Akizungumza juu ya mkataba huo Aveva alisema mkataba huo utaongeza chache ya mafanikio ya timu yao kwa kuwa walikuwa na matatizo ya uendeshaji wa klabu kutokana na mapato kiduchi yaliyotokana na vyanzo vichache.
Akizungumzia kuhusu mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji waSportPesa Tanzania, Abbas Tarimba alisema:
“Tumesaini mkataba wa miaka mitano, tumeshazungumza na Simba fedha hizi za udhamini zitumike kwa maslahi ya klabu kweli na zitahakikiwa na wao wenyewe, mwaka wa kwanza wa mkataba watapata shilingi milioni 880, ambapo kila mwaka wa mkataba kutakuwa na ongezeko la asilimia tano ya kiasi hicho
0 comments:
Post a Comment