Bi. Juliet Kairuki aliteuliwa na Rais mstaafu wa Tanzania Mhe Jakaya Kikwete kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha uwezeshaji (TIC) April 2013.
Kabla uteuzi huo Juliet Rugeiyamu Kairuki amefanya kazi Afrika Kusini kwa miaka 12 ambapo miaka 10 alikua kati sekta ya benki akiwa Meneja Mkuu wa Chama cha Mabenki Afrika Kusini (General Manager of the Banking Association South Africa).
Juliet Kairuki ni Mwanasheria mwenye shahada ya kwanza na ya uzamili kwenye sheria. Alipomaliza shahada ya kwanza alifanya kazi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla ya kwenda nchini Afrika Kusini alikokwenda kusomea shahada ya uzamili.
Juliet Kairuki ni mtaalamu wa miradi ya Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi (Public-Private Partnership). Kati ya mwaka 2002 na 2008 alikuwa Meneja wa Mradi wa Public Private Partnership Capacity Building in SADC, katika Chama cha Mabenki cha Afrika Kusini (The Banking Association South Africa).
Kuanzia mwaka 2008 hadi wakati anateuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji TIC alikuwa Meneja Mkuu wa Idara ya Benki na Huduma za Fedha katika taasisi hiyo.