Jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea klabu ya Real Madrid yaHispania Cristiano Ronaldo limerudi tena kwenye headlines leo Jumatano ya April 28 2016. Ronaldo amerudi kwenye headlines baada ya Real Madrid kudaiwa kutoa ripoti ya maendeleo ya majeruhi yake.
Ronaldo ambaye amekosa mechi mbili za Real Madrid huenda akakosa michezo mingine ikiwemo mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Man City utakaochezwa Santiago Bernabeu, Ronaldo anadaiwa kupimwa na MRI Scan na kukutwa ana tatizo la msuli (muscle tear).
Cristiano Ronaldo ambaye alikosa michezo miwili iliyopita ya Real Madrid, aliumia katika mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Villarreal April 20 2016, hadi sasa Ronaldoamefunga magoli 47 msimu huu katika mechi 45 alizoichezea Real Madrid na kuwa mchezaji wa kwanza wa Real Madrid kufunga magoli mengi kwa msimu.
0 comments:
Post a Comment