www.kenethngamoga.blogspot.com

Dubai imepiga marufuku wanawake waja wazito kuvuta ama hata kuingia katika migahawa inayouza Shisha .Hatua hiyo inafuatia shinikizo la kuimarisha afya ya umma na haswa afya ya mama waja wazito.Sheria hiyo inawadia baada ya kampeini ya kuwazuia wanawake wajawazito kuingia pahala panapovutiwa sigara jarida la aGulf News linasema
Kampeini hiyo inayoendeshwa kwa kutumia mabango na picha ya mwanamke mjamzito akiambiwa na mwanaye aliyeko tumboni kuwa ''Uamuzi wa kuvata au la ni wako,,,sio wangu''
Mabango hayo yanaeleza kuwa watoto ambao hawajahitimu miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta shisha au sigara.
Image copyright
"Kauli hiyo ni ya serikali wala sio hoja ya kujadiliwa na yeyote '' alisema mkurugenzi wa afya ya umma wa Dubai bwana Marwan Al Mohammed.
Wamiliki wa vilabu vya burudani vinavyouza shisha wamekuwa wakilalamikia kutokuwepo kwa sheria zinazoharamisha wanawake wajawazito kutoingia katika vilabu hivyo.
''Sasa sheria hii inaweka bayana anayeruhusiwa kisheria kuvuta ima ana pesa au la '' aliongezea kusema.
Mwaka wa 2014 milki hiyo ya kiarabu ilipitisha sheria kali dhidi ya uvutaji wa sigara ambayo ilipiga marufuku matangazo ya aina yeyote ya kibiashara ya Sigara.
Image captionMabango hayo yanaeleza kuwa watoto ambao hawajahitimu miaka 18 na wanawake wajawazito hawaruhusiwi kuvuta shisha au sigara.
Vilevile sheria hiyo ilipiga marufuku uvutaji wa sigara ndani ya gari iwapo mna mtoto mwenye chini ya umri wa miaka 12.
Aidha sasa kuna sheria inayotoa mwelekeo ya ni wapi shisha itauzwa na itaruhusiwa kuwepo umbali gani kutoka kwenye makazi ya watu.
Chanzo BBC
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment