Mapigano ya wakulima na wafugaji Morogoro kata ya Hembeti ,Kijiji cha Kigurukwa,Kitongoji cha Dihamba chasababisha mauaji ya mbuzi 75 waliokatwakatwa kwa mapanga, Waziri wa Kilimo,Uvuvi na Mifugo bila kuchelewa awasili eneo la tukio na kuchukua hatua
Mh. Mwigulu Nchemba ameagiza kamati ya Ulinzi ya mkoa na wilaya kuhakikisha waliofanya uharibifu huo wakamatwe haraka sana.
Pili ameagiza kupitia hukumu ya mahakama iliyotolewa mwaka 2015 kuweka mipaka kati ya eneo la wakulima na wafugaji itekelezwe haraka iwezekanavyo.
Mwisho Waziri Mwigulu Nchemba ameagiza kuwepo mkutano wa hadhara wa wakulima na wafugaji na viongozi wote wa serikali wa wilaya na mkoa tarehe 20/02/2016 ndani ya kata ya Hembeti.
0 comments:
Post a Comment