Gazeti la Mtanzania leo March 22 limeripoti kuhusu kamati za Bunge kutarajiwa kufanyiwa mabadiliko makubwa baada ya ripoti ya uchunguzi wa mwenendo wa wabunge kuwatuhumu baadhi yao kujihusisha na vitendo vya rushwa kutua mezani kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa facebook kuwa….
>>>’Kuna tuhuma za rushwa dhidi ya Kamati mbalimbali za Bunge ikiwemo kamati ninayohudumu. Nimemwandikia Spika Kuomba Uchunguzi juu Ya tuhuma hizo na kwamba achukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayekutwa kuhusika na vitendo vya rushwa. Nimejiuzulu Ujumbe wa Kamati ili Kutoa Nafasi Ya Uchunguzi Husika‘
Zitto pia amezungumza na Kito cha ITV na kufafanua zaidi maamuzi yake hayo ambapo amesema..
>>>’ni vizuri spika aagize uchunguzi wa vyombo vya dola, vyombo vya dola vikishachunguza ndio hatua ziweze kuchukuliwa kwa sababu kuhamisha tu watu kwenye kamati haisadii kuweka misingi ya utawala bora’:-Zitto Kabwe
>>>’tuhuma hizi ni nzito na imekuwa ni kawaida hasa kwa wabunge kutuhumia na mambo yamekuwa yakiishia juu juu bila hatua kuchukuliwa na hiyo imekuwa ikishusha hadhi ya bunge kwa hiyo ni vizuri kuhakikisha kwamba jambo ili linafanyiwa uchunguzi wa kina, ningetaka wabunge wakubali ili tuchunguzwe ili vyombo vya dola viweze kudhibitisha tuhuma hizi na hatua sitahiki ziweze kuchukuliwa kwa watu watakaokutwa na makosa’:–Zitto Kabwe
0 comments:
Post a Comment