www.kenethngamoga.blogspot.com

Samatta Aing'arisha stars Chad

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika  (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.
Maguli 6Mbwana Samatta akivaa kitambaa cha unahodha kwa mara ya kwanza, amekiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kupata ushindi wa goli 1-0 ugenini dhidi ya Chad kwenye mchezo wa Group G kuwania nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Afrika inayotarajiwa kufanyika mwaka 2017 nchini Gabon.
Mbwana Samatta amefunga goli hil kipindi cha kwanza akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Farid Musa goli ambalo limedumu hadi dakika 90 za mchezo huo.
Stars imefikisha pointi 4 baada ya kucheza michezo 3, matokeo hayo yanaifanya Stars ifikishe idadi sawa ya pointi na Nigeria ‘The Super Eagles’ lakini Stars ipo mbele ya Nigeria kwa mchezo mmoja. Nigeria itakutana na Misri kwenye mchezo wa kundi ilo siku ya Ijumaa.
Stars itacheza mchezo wake wa marudiano dhidi ya Chad siku ya Jumatatu March 28 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Matokeo ya mechi nyingine za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa mechi ambazo tayari zimemalizika yapo kama ifuatavyo:
Guinea-Bissau 1-0 Kenya
South Sudan 1-2 Benin
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment