www.kenethngamoga.blogspot.com

''Mimi sijichubui bhana''-Ray Kigosi


Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi .
Ray ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
Naye Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.
Katika kipengele cha ''Cheche'' ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.
Pia wamemtaka mwigizaji huyo kuwa na moyo wa kusaidia wasanii chipukizi ilikukuza tasnia ya uigizaji hapa nchini
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment