www.kenethngamoga.blogspot.com

MKOA WA MOROGORO WAONGOZA KWA KUFELI (MATOKEO KIDATO CHA NNE)

Masaa kadhaa tangu baraza la mtihani la taifa la Tanzania NECTA kutangaza matoko ya kidato cha nne ambapo Mikoa ya Kanda ya Ziwa imeendelea kuongoza kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne baada ya shule zake nne za sekondari kuingia kwenye kumi bora ya matokeo ya mwaka 2015, zikiongozwa na Kaizerege iliyoshika nafasi ya kwanza kwa mara ya pili mfululizo.


Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Kaizerege ya mkoani Kagera inaongoza shule za mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo pia inajumuisha shule za Alliance Girls, Alliance Boys na Alliance Rock Army zote za Mwanza ambazo kwa pamoja zimetoa wanafunzi 237 waliofaulu.

Mikoa hiyo inafuatiwa na Kanda ya Mashariki, ambayo ina shule tatu kutoka mikoa ya Dar es Salaam (Canossa, Feza Boys na Girls) na (Marian Boys) ya Pwani, wakati shule nyingine zinazoingia kwenye orodha hiyo zinatoka mikoa ya Mbeya (St Francis) na Kilimanjaro (Uru Seminary).
Shule ya Kaizerege ilishika nafasi ya kwanza mwaka 2013 kwenye matokeo ya kidato cha nne kwa shule zilizokuwa na idadi ya wanafunzi chini ya 40, lakini mwaka jana ikaibuka tena kidedea ikiwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Mwaka huu, wanafunzi wote 72 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza, isipokuwa mwanafunzi mmoja tu ambaye hakufanya mtihani.

Shule ya Sekondari Canossa imejiwekea historia baada ya kutoa mwanafunzi bora, Butogwa Charles Shija na kushika nafasi ya tano kwenye orodha ya shule kumi zilizofanya vizuri.

Mkuu wa shule hiyo, Sista Irene Nakamanya alisema wameingia kwenye nafasi hiyo kutokana na wanafunzi kuwa na hofu ya Mungu.

“Ni hofu ya Mungu. Tunapokea watoto wa dini tofauti. Tunawalea kwa hofu ya Mungu. Pili, nidhamu na juhudi za wanafunzi na walimu ambao huwaangalia wanafunzi kama darasa na mmoja mmoja ili kuwasaidia,” alisema Sista Irene.

Hakuna shule kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyo kwenye orodha ya shule kumi zilizoshika mkia, badala yake Kanda ya Mashariki ndiyo ‘imetamba’ kwa kutoa shule sita, huku mbili zikiwa mkiani, kwa mujibu wa matokeo hayo.

Shule iliyoshika mkia ni Malinyi ya Morogoro, ikifuatiwa na Kichangani pia ya Morogoro, wakati ya tatu kutoka mkiani ni Gubali ya Dodoma.


Shule ya Sekondari Saviak ya Dar es salaam imeshika nafasi ya nne kutoka mkiani, ikifuatiwa na Patema (Tanga), Kuriji (Pwani), Sofi (Morogoro), Korona (Arusha), Igawa (Morogoro) na Pande ya Lindi.

Baada ya matokeo hayo kuonyesha mkoa wa morogoro ndio wa mwisho kitaifa huku Shule iliyoshika mkia ni Malinyi ya Morogoro, ikifuatiwa na Kichangani pia ya Morogoro kupitia mitandao ya kijamii wadau mbali mbali waonyesha masikitiko yao

BAADHI YA MAONI





NIMEUMIZWA SANA NA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE KUONYESHA MKOA WANGU WA MOROGORO UMESHIKA NAFASI YA MWISHO...
Posted by Dismas Lyassa on Thursday, February 18, 2016
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment