John Woka ni msanii ambaye Tanzania ilikuwa nae sana kwenye chati za muziki wa
bongofleva kupitia kundi la Watukutu, na sasa Tanzania imepata taarifa za kifo chake
ilichotokea alfajiri ya February 16 ikiwa ni saa kadhaa tu
John Woka ni msanii ambaye Tanzania ilikuwa nae sana kwenye chati za muziki wa bongofleva kupitia kundi la Watukutu, na sasa Tanzania imepata taarifa za kifo chake kilichotokea alfajiri ya February 16 ikiwa ni saa kadhaa tu baada ya kupelekwa Hospitali.
Woka amefariki baada ya kupata ajali wakati anatengeneza gari Sinza kwenye mfumo wa AC inasemekana kuna kitu kilifyetuka baada ya kufungua AC na kumpiga kwenye paji la uso na kuingia kama inchi 3 au 2 hivyo damu nyingi zikaanza kumtoka kichwani na mpaka anafikishwa hospitali, Woka alikuwa katika chumba cha wagonjwa Mahututi.
Kifo cha John Woka ni pengo jingine kwenye bongofleva, alipita kwenye chati mbalimbali za muziki huu kutokana na nyimbo zake kama mganga na hii kitu hii ambazo alizipiga kwa kurap kama mlevi
SIKILIZA MOJA YA NYIMBO ZA JOHN WOKA HAPA CHINI
0 comments:
Post a Comment