Usiku wa February 16 kuamkia February 17 jamaa ambaye jina lake lilizidi kukua baada ya ushindi wa shindano la Big Brother Idris Sultan, aliingia kwenye headlines baada ya kupost picha Instagram yenye watoto mapacha, lakini aliambatanisha picha hiyo na maneno ambayo yanaonesha huzuni ya kupoteza watoto mapacha. Idris aliandika ujumbe unaosomeka kwa lugha ya kiingereza, lakini tafsiri yake ni kuwa alikuwa anatarajia kupata watoto mapacha ila ujauzito umeharibika wa muhusika aliyetarajia kuzaa nae.
lakini aliambatanisha picha hiyo na maneno ambayo yanaonesha huzuni ya kupoteza watoto mapacha. Idris aliandika ujumbe unaosomeka kwa lugha ya kiingereza, lakini tafsiri yake ni kuwa alikuwa anatarajia kupata watoto mapacha ila ujauzito umeharibika wa muhusika aliyetarajia kuzaa nae.
Hivi ndivyo unavyosomeka ujumbe wa Idris kwa lugha ya Kiswahili
Kwa mapacha wangu ambao walikuwa bado hawajazaliwa
“Ni haraka sana mmeingia katika mfumo wa maisha yetu, lakini ni haraka pia mmetuacha, sikuwahi kupata nafasi ya kukutana na nyinyi, nina vingi nataka niseme ninavyofikiria ndani ya kichwa changu vinatosha kunifanya mwendawazimu, ukizingatia mmeishi kwa wiki sita pekee, tuliwapenda sana na natamani ningepata nafasi ya kuwashika, mungu ametoa na mungu ametwa kama ambavyo amepanga na hatuwezi kulalamika huenda ametuandalia mengine mazuri zaidi”
Idris Sultan kupitia vyombo vya habari kadhaa aliripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mrembo kutoka kiwanda cha filamu Bongo, lakini pia ni Miss Tanzania wa mwaka 2006 Wema Sepetu, kabla ya baadae mwenyewe kukiri kuwa katika mahusiano na Wema
0 comments:
Post a Comment