Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imewataka
wasimamizi wa uchaguzi na jeshi la polisi kutenda haki siku ya uchaguzi
mkuu Oktoba 25 mwaka huu kwa vyama vyote.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva.
Rai
hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na mwenyekiti wa NEC Jaji
mstaafu Damian Lubuva katika mkutano wa pamoja kati ya NEC na wasimamizi
wa uchaguzi nchi nzima pamoja na Jeshi la polisi na kuongeza kuwa kama
watendaji hao wakitenda haki na haki ikaonekana kutendeka basi Uchaguzi
utakuwa huru na haki na hivyo kudumisha Amani na kuiepusha nchi na
machafuko.
Kwa upande wa mkurugenzi msaidizi wa uchaguzi wa NEC Emmanuel Kawishe amesema makosa yote ya kiufundi yaliyotokea wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa mfumo wa BVR yanafanyiwa kazi pamoja na kuhakiki majina yote ili kutoa daftari lililokamilika siku 8 kabla ya Uchaguzi.
Kawishe ameongeza kuwa watu ambao vitambulisho vyao vimepotea hawatapiga kura na kila mtu atapiga kura pale tu alipojiandikisha.

0 comments:
Post a Comment