Vijana mkoani Iringa wamekumbushwa kufuatilia na
kuchambua sera za vyama vya siasa katika kipindi hiki cha kampeni ili
kuepukana na vitendo vya rushwa toka kwa wagombea.
Mwanasheria wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy
Afisa
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) makao
makuu jijini Dar-es Salaam Bi Dorothea Mrema amesema vijana wanaweza
kuchagua viongozi bora ikiwa watasikiliza na kuzielewa vema sera za
vyama husika.
Aidha, mwanasheria wa TAKUKURU Bi. Restituta Kessy amevikumbusha vyama vya siasa na wagombea kuzingatia sheria za uchaguzi.
Hata hivyo, mmoja wa maafisa hao wa TAKUKURU kutoka makao makuu Bi. Sarah Chodata amewashauri vijana kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 25 ili kupata viongozi waadilifu.

0 comments:
Post a Comment