Siku 11 zimebaki kuifikia October 25 2015, ambapo Tanzania itakuwa kwenye tukio jingine kubwa na la kihistoria, Watanzania Milioni 22.7 waliothibitishwa na Tume ya Uchaguzi NEC, watapiga Kura kuchagua Viongozi katika ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Kwa sasa bado mchakamchaka wa Kampeni kwenye Majukwaa ya Siasa bado unaendelea, jana October 12 2015 Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA ambaye anawakilisha umoja wa wa Vyama vya UKAWA, Edward Ngoyai Lowassa alitua kwa mara nyingine kwenye Viwanja vya Furahisha, ndani ya Mwanza kwa ajili ya kuendelea na Kampeni zake.
0 comments:
Post a Comment