Kampeni za kuwania nafasi ya Urais nchini Tanzania imeendelea kushika katika Sehemu mbalimbali huku wagombea wawili wenye upinzani mkali wakiiteka mikoa waliyotembelea kwa kulakiwa na Umati wa watu.
Mgombea Urais wa Ukawa kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa Jijini Mwanza.
Akiwa Jijini Mwanza mgombea urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa ambaye alihutubiwa katika viwanja vya furahisha ambavyo vilifurika umati wa watu aliwaahidi wakazi wa jiji hilo kuleta maendeleo kupita sekta mbalimbali.
Kwa upande wake Mgombea Urais wa Chama chama cha Mapinduzi (CCM) alikua mkoani Lindi ambapo aliongozwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho aliwaambia wakazi wa mkoa huo kufanya uamuzi wa sahihi wa kumchagua mtu muadilifu asiekuwa na kashfa yoyote ya Ufisadi.
Naye mgombea pekee Mwanamke katika kinyang'anyiro hicho kama Rais kamili akiwakilisha chama cha ACT-Wazalando alikuwa mkoani Dodoma ambapo aliwaahidi wakazi wa vijiji alivyotembelea kudumisha kilimo ili kuinua uchumi.
Kwa upande wake mgombea wa urais kupitia CHAUMMA, Hashim Rungwe akiwa katika jimbo la Ubungo jijini Dar es salaam amesema kuwa atafufua viwanda ili kuweza kuendeleza uchumi wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment