Baada ya kutangaza kuvunjwa mkataba Dar es Salaam Young Africans na kocha wake wa zamani ambaye walimpatia majukumu mapya ya kuwa mkurugenzi wa ufundi raia wa Uholanzi Hans van Pluijm, leo March 17 2017 timu ya Singida United iliyopanda kucheza Ligi Kuu imempa mkataba wa miaka miwili kocha huyo.
Baada ya taarifa hizo kuenea aliyekuwa afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika ujumbe unaotafsirika kama kumfariji kocha Hans van Pluijm “Babu Hans pumzika hapo kwa muda, wapiga dili wanaomdanganya muhindi wakishaondoka kule, tutarejea tu hata kwa mlango wa uani”
Kuondolewa kwa Hans van der Pluijm akiwa kaipatia Ubingwa wa Ligi Kuu na FA Yanga msimu uliyopita sambamba na kuiwezesha kufika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la shirikisho barani Afrika, kumewashangaza wengi kutokana na kutoona sababu za msingi za kumuondoa Han
s
s
0 comments:
Post a Comment