Kwa upande wa Real Madrid wao waliingia uwanjani bila ya uwepo wa staa waoCristiano Ronaldo ambaye bado anaendelea kuuguza jeraha lake la goti, kukosekana kwa Ronaldo hakukuwa pigo sana kwani Real Madrid walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-2 ndani ya dakika 120, hiyo inatokana na dakika 90 kumalizika kwa sare 2-2.

Mchezo haukuwa rahisi kwa Real Madrid kwani mashabiki wao walikata tamaa kutokana na mchezo hadi dakika ya 89 walikuwa nyuma kwa goli 2-1 ila dakika ya 90 Sergio Ramos akaisawazishia Real, licha ya Real Madrid kuanza kupata goli dakika ya 21 kupitia kwa Marco Asensio.
Sevilla walifunga goli zao mbili kupitia kwa Vazquez dakika ya 41 na Konoplyankadakika ya 72 kwa mkwaju wa penati, baada ya kuongezwa dakika 30 na kuufanya mchezo kuchezwa kwa dakika 120 mechi ilizidi kuwa ngumu kwa pande zote ila Real Madridwalikuwa na bahati zaidi kuliko Sevilla kwani dakika moja kabla ya mchezo kumalizikaDaniel Ramos alipachika goli lililoipa ubingwa Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment