Unapokuwa unafanyakazi sehemu yenye wafanyakazi wengi ni dhahiri kuwa kuna mmoja atakuwa yupo karibu na bosi na mara nyingi huyu hupendwa kwa sababu mbalimbali na mara nyingi bosi hutamani kumsaidia huyu ili azidi kuinuka zaidi.
Wataalamu wa masuala ya kazi wanaeleza kuwa, kadiri utakavyokuwa unapendelea na bosi na kujitenga na wengine wakati wingine unajitengenezea mazingira ya kukosa msaada kutoka kwa wenzako.
Ikifika mahali ukiona bosi wako anakupendelea wewe shukuru, kuwa mnyenyekevu, fanya vitu kwa unyenyekevu na mambo yanapokuwia magumu, zungumza na bosi wako.
Hizi hapa ni dalili 12 kuwa bosi wako anakupendelea wewe
Anakujumuisha katika vikao vingi kuliko wafanyakazi wenzio.
Hii ni ishara muhimu, inaonyesha wanaheshimu mawazo yako na mchango wako na wanatambua kwamba una mchango chanya kwa kufanyakazi. “Hakuna mtu anafurahia kuwa katika mikutano na watu hathamini kile anachosema. Hivyo ukiona mchango wako unakubalika ni ishara nzuri.
2. Wanakujumuisha katika mipango mikubwa na nyeti.
Kama wewe hua unashirikishwa kwenye miradi mikubwa ya kampuni na mingine ni ya siri basi wewe bosi anakupendelea. Wewe umekuwa ni mtu wa mradi baada ya mradi. Bosi wako atakua anaiamini kazi yako kuwa kila ukifanya mradi basi mafanikio yanaonekana.
3. Anakutumia wewe wakati mambo yanapokwenda mrama
Kama kila tatizo linapotokea wewe ndio huwa ni mtu wa kwanza bosi wako kukufikiria ukaweke mambo sawa, basi anaamini utendaji kazi wako.
4. Huwa anakutaka umbatane naye anapokwenda nje ya mji au kwenye mikutano.
Kwa mara nyingine, hii huonyesha kuthaminika kwa ulichonacho na kuendelea kupata uzoefu unapokuwa na bosi wako na kuendelea kujijenga kwa kujifunza mambo mapya kwa ajili ya kazi yako.
5. Anahitaji ushauri wako mara kwa mara kuliko anavyohitaji kutoka kwa mtu mwingine
Kitendo cha bosi wako kukuomba ushauri hakika ni ishara kubwa sana kuwa ndani ya moyo wake anathamini mchango wako, hekima na taaluma yako. Kama wewe pekee ndiye unayeombwa ushauri, basi hiyo ni ishara kuwa wewe ni bora.
6. Unapewa nafasi ya kuzungumza kwa niaba
Bosi akikuruhusu wewe kusimama na kuzungumza moja kwa moja kwa niaba yake, ni sawa na amekupa nafasi yake, na hawezi kufanya hivyo kama anajua wewe ni kichwa resi maana anajua utamuaibisha. Wakati mwingine hata ukizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzio hata kama unamkosoa bosi, atasikiliza.
7. Una uhuru wa tofauti
Kuna wakati unajikuta kuwa huna uangalizi mkali kwenye kazi zako kama walivyo wafanyakazi wengine, au hata ukizungumza hukosolewi kama wengine. Wakati mwingine unajikuta kuwa mambo unayoyafanya yanashabihiana sana na anayoyafanya bosi tofauti na yanavyoshabihiana na wafanyakazi wenzako. Ukiona hivyo jua kuwa bosi ameshakuinua.
8. Haupangiwa wakati wa kufanyakazi.
Kama ukijikuta kuwa hausimamiwi sana na kuambiwa hapa fanya hivi au vile, unakuwa unatumia maamuzi yako wewe mwenyewe na kufanya vitu ambavyo wakati mwingine ni hatari hiyo ni ishara kuwa uko katika kitabu cha watu wema cha bosi wako.
9. Anakwambia mambo yaliyotakiwa kuwa siri.
Kuna mambo mengine kwenye kampuni hutakiwa kuwa siri kwa viongozi tu, lakini wakati mwingine bosi anaweza akakuambia na akakutaka na wewe usimwambie mtu. Hii inaonyesha kuwa anakuamini.
10. Anakwambia mambo yake binafsi.
Kama bosi wako anatumia muda wake kukuambia kuhusu mambo ya familia yake na mambo yake mengine kuliko mtu mwingine yeyote, ambayo hayahusu kazi, ni dhahiri kuwa wewe ni mtu wa karibu kwake na anakuamini.
11. Huogopi kufanya kitu kipya ambacho huenda ni cha hatari.
Kama unaweza kufanya kitu kipya katika kampuni ambacho pengine ukikosea ni hatari kubwa na ni ishara kuwa wewe unapendelewa na bosi kwani kama mtu hana uhusiano mzuri na bosi wake hatathubutu. Hii ni ishara kuwa bosi amekupa uhuru na anakuamini kuwa hutaharibu kwenye kile unachokifanya kuwa kitafanikiwa.
12. Anakuwa mwenye furaha unapokuwa naye.
Wakati mwingine bosi wako anakualika katika matukio ya kijamii yanayohusu familia yake sababu mnakuwa mnaendana. Mara kadhaa mnapokuwa pamoja manafanya mambo kwa kuelewana na yanakwenda sawa, hii ni ishara kuwa bosi wako anakupendelea wewe.
0 comments:
Post a Comment