Zikiwa zimebaki mechi 13 kabla ya kumaliza msimu wa ligi kuu nchini Uingereza ..kocha Mkuu wa mabingwa wa EPL 2015_2016 Claudio Ranier Amefutwa kazi
Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri amefukuzwa kazi, miezi tisa baada ya kushinda Ligi Kuu ya England.
Leicester wako pointi moja tu juu ya timu zilizopo hatarini kushuka daraja huku zikiwa zimesalia mechi 13.
"Bodi kwa uzito mkubwa inahisi kuna ulazima wa kubadili uongozi. Ingawa ni uamuzi mgumu lakini ni muhimu kwa maendeleo ya timu" imesema taarifa ya Leicester.
Ranieri, 65, aliipeleka Leicester kunyakua ubingwa licha ya wengi kutowapa nafasi hiyo.
0 comments:
Post a Comment