Mbunge wa Mikumi kupitia ticket ya CHADEMA Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay ametumia time yake kuandika machache ya moyoni baada ya mbunge mwenzake wa CHADEMA, Peter Lijualikali kuhukumiwa kwenda jela miezi 6.
Lijualikali amepewa adhabu hiyo kutokana na kukutwa na hatia ya kuwafanyia Polisi fujo wakati wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa halamshauri ya wilaya ya kilombero mwaka 2016.
Profesa Jay ameandika >>> ‘Wanadhani wanatutisha ili tuogope na kurudi nyuma, hawajui kuwa wanatukomaza na kutuongezea ujasiri zaidi wa kuendeleza mapambano.. ipo siku tutaelewana tu na jela tutaona kama tumekwenda DISCO, hongera mpiganaji @mh.lijualikali hatujui kesho ni zamu ya nani ila WE ARE VERY READY!! TRUST ME..
ALUTA CONTINUA. .
ALUTA CONTINUA. .
0 comments:
Post a Comment