Kama ni mfatiliaji wa familia ya Bw. Nasib (Diamond) Abdul basi utakuwa tayari ushaona utofuti uliopo baina ya watoto wake wawili, hapa namzungumzia Princess Tiffah pamoja na Prince Nillan.
Kipindi mwanae wa kike Tiffah, baada ya kuzaliwa alikuwa ni mtoto ambae kapokea shamra shamra nyingi za hatari kutoka kwenye familia yake na kupata deal kubwa za matangazo katika umri mdogo lakini kwa Nillan ambe ni mdogo wake na Tiffah imekuwa si hivyo tulivyotarajia kuoa tulio wengi.
Je ni kwanini mbwembwe zilizo kuwepo kwa Latifah hazijawa kwa Nillan?
Akipiga story na Clouds E! ya Clouds Tv, Diamond alisema “Wanawake wameumbiwa mashauzi ndio maana Tiffah tumemshauzisha, lile ni dume (Nillan) linawinda, kwanza jina lake kutoka ilikuwa tatizo, tunabishana kila mtu anataka jina lake, mpaka kuja kupata Nillan, kuna pia Daillan, yote ni majina yake”.
Mbali na hilo pia Diamond alizungumzia kuhusu 40 ya Nillan, ambapo alisema “Atakuwa na 4o yake ambayo itafanyika South Afrika, so tutatoka hapa tutaenda South Afrika kwa ajili hiyo”.
Mtoto huyo alizaliwa saa 10 na dk 35 Alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki, Jumanne, December 6.
Mpaka sasa Mtoto wa pili wa Diamond Platnumz, Prince Nillan ameendelea kuwa maarufu katika mtandao wa kijamii wa Instagram baada ya kufikisha followers 76.1k ikiwa Mtoto wa kwanza wa muimbaji huyo, Princess Tiffah ana followers milioni 1 katika mtandao huo.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na
Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata
habari mpya.
0 comments:
Post a Comment