Soka la Tanzania leo December 4 2016 limepata pigo kutokana na kupokea taarifa za kifo cha mchezaji wa timu ya Mbao FC chini ya umri wa miaka 20 Ismail Khalfan aliyekuwa sehemu ya kikosi cha Mbao FC kilichocheza dhidi ya Mwadui FC.
Ismail Khalfan amepoteza maisha katika michuano ya timu za vijana wa umri chini ya 20 katika mchezo wa mwisho wa round ya 7 Kundi A kituo cha Kaitaba Bukoba, Ismail Khalfan alikuwa anavaa jezi namba 4 katika mashindano hayo.
Katika mchezo huo ambao Mbao FC walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya timu ya Mwadui FC (U20), Ismail Khalfan alifunga goli la kwanza katika ushindi huo kabla ya kipindi cha pili kugongwa na kutolewa kukimbizwa hospitali ya rufaa Bukob
a
a
0 comments:
Post a Comment