Chama cha soka England FA leo December 5 2016 kimetangaza kumfungia mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea timu ya Manchester City Sergio Aguero, mshambuliaji huyo amefungiwa mechi 4 kutokana na kadi nyekundu aliyooneshwa wakati wa mchezo dhidi ya Chelsea.
Aguero mwenye umri wa miaka 28 wakati wa mchezo wa Man City dhidi ya Chelsea alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea faulo beki wa Chelsea David Luiz katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Etihad na Man City kupoteza kwa goli 3-1, Aguero atakosa mechi za Leicester, Watford, Arsenal na Hull.
Hii sio mara ya kwanza Aguero kuingia katika matatizo kama hayo aliwahi kukumbana na kadi nyekundu August kwa kumpiga kiwiko Winston Reid wa West Ham, Fernandinho pia kafungiwa mechi 3 kutokana na kosa alilofanya la kumsukuma Cesc Fabregas na kuoneshwa kadi nyekundu
,
,
0 comments:
Post a Comment