Kama ni shabiki wa klabu ya Real Madrid hususani mchezaji Gareth Bale ambaye ni moja kati ya wachezaji ghali zaidi duniani, taarifa hii ikufikie ambayo imetolewa leo kuhusu staa huyo wa kimataifa wa Wales anayeichezea Real Madrid ya Hispania.
Taarifa iliyotolewa leo kuwa Bale atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne, kufuatia upasuaji wa enka ya mguu wa kulia atakaofanyiwa kutokana na jeraha lake alilolipata katika mchezo wa UEFA dhidi ya Sporting CP uliomalizika kwa Real Madridkuibuka na ushindi wa goli 2-1.
Bale atafanyiwa upasuaji London na kuna uwezekano akaukosa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la dunia March 24 kati ya Wales dhidi ya Ireland utakaochezwa Dublin, Wales kwa sasa wapo nafasi ya 3 Kundi D linaloongozwa na Ireland akifuatiwa na Serbia kwa tofauti ya point 2
.
.
0 comments:
Post a Comment