www.kenethngamoga.blogspot.com

Timu ya Samatta KRC Genk Yatinga hatua inayofuata Europa League

Usiku wa leo November 24 2016 timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samattailicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.
Usiku wa leo November 24 2016 timu ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ilicheza mchezo wake wa tano wa hatua ya Makundi ya UEFA Europa League dhidi ya timu ya Rapid Wien ya Austria.
KRC Genk katika mchezo huo wa tano walikuwa nyumbani katika uwanja wao wa Luminus, Genk wakiwa nyumbani walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 55 dhidi ya wageni wao Rapid Wien, kitu ambacho kimewasaidia kuibuka na ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Nikolaos Karelis dakika ya 11.


Kwa matokeo hayo Genk na Atletico Bilbao wanafuzu hatua inayofuata kutokana na wote kuwa na point 9 wakati Rapid Wien na Sassuolo ya Italia watakuwa wanasubiri mchezo wa mwisho wa kukamilisa ratiba, maana hata wakishinda watakuwa na point nane kila mmoja, point ambazo hazitoshi kuipiku Genk wala Atletico Bilbao.

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment