Klabu ya TP Mazembe ya Jahmhuri ya Kidemokrasia ya Kongo October 23 2016 ilitangaza rasmi kupitia tovuti ya klabu hiyo kuwa mtanzania Thomas Ulimwenguamemaliza mkataba na TP Mazembe, lakini Ulimwengu hajataka kuongeza mkataba mwingine.
TP Mazembe kupitia tovuti yao wameeleza kuwa Ulimwengu amemaliza mkataba wa miaka mitano wa kuitumikia klabu hiyo, lakini wameweka wazi kuwa walimuhitaji lakiniUlimwengu amekataa kufanya mazungumzo ya kuongeza mkataba na anataka kuondoka.
Mapema mwaka huu Thomas Ulimwengu aliongea na AyoTV kutoka Lubumbashi na kuweka wazi kuwa anamalizana na TP Mazembe mwishoni mwa mwaka huu, hivyo kwa sasa malengo yake ni kufuata nyayo za rafiki yake Mbwana Samatta kwenda kucheza soka Ulaya
.
.
0 comments:
Post a Comment