Gavana wa benki kuu, Prof. Benno Ndulu wakati akielezea taarifa ya hali ya kiuchumi nchini amesema thamani ya Shilingi imeendelea kuwa tulivu katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, kufuatia hatua mbalimbali za sera ya fedha zilizochukuliwa na Benki Kuu katika kusimamia hali ya ukwasi kwenye uchumi pamoja na mwenendo wa uchumi ndani na nje ya nchi.
Prof. Ndulu amesema thamani ya shilingi itaendelea kuimarika kutokana na kuimarika kwa sekta ya nje kulikotokana na ongezeko la mauzo ya bidhaa na huduma nje ya nchi. Aidha ameongeza kuwa kupungua kwa thamani ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje kumechangia katika utulivu wa thamani ya shilingi.
>>>’Kwenye upande wa thamani ya shilingi huko pia sasa karibu mwaka mzima, shilingi ya Tanzania iko stable na kwa siku za karibuni imeimarika kidogo na matarajio yetu shilingi itabakia kuwa stable kwasababu ukuaji wa mauzo ya nje bado umeendelea kuwa mzuri katika nusu mwaka ya kwanza mauzo ya bidhaa za huduma nje ya nchi yameendelea kukua mpaka kufikia asilimia 14.2.’;-Prof. Ndul
u
u
0 comments:
Post a Comment