Leo Jumatatu October 24, 2016 Mtu wangu nakuletea List ya kwanza yenye majina ya wanasoka mastaa watakaowania tuzo ya mwanasoka bora wa Ballon D’Or. Tayari majina ya kwanza ya wanasoka wanaofanya vizuri kwenye game yametajwa huku Cristiano Ronaldo na Garret Bale wakiwemo.
Mastaa hao kutoka Club ya Real Madrid wanaungana na wanasoka wengine Sergio Aguero, Pierre-Emerick Aubameyang pamoja na Gianluigi Buffon kwenye list ya wanasoka 30 watakaowania tuzo hii kubwa kutoka FIFA.
Tuzo hii ya Ballon d’Or pamoja na ile ya FIFA World Player of the Year ziliunganishwa mwaka 2010 na ikapatikana tuzo moja ya FIFA Ballon d’Or, lakini muungano wa tuzo hizi unaisha mwaka huu, na kila moja itakua ikitolewa kivyake.
0 comments:
Post a Comment