Wavulana wawili pacha ambao walikuwa wameshikana vichwani wametenganishwa na madaktari mjini New York, Marekani.
Jadon na Anias McDonald wa umri wa miezi 13 walifanyiwa upasuaji uliochukua saa 16 katika hospitali ya Montefiore.
Kwa sasa wanafanyiwa matibabu ya kuwezesha mafuvu ya vichwa vyao kukua na kujaza pengo lililoachwa.
Mama yao Nicole McDonald aliandika kwenye Facebook Ijumaa asubuhi jinsi alivyokuwa na furaha lakini pia na "uchungu kuhusu mustakabali wa watoto hao."
Alipakia picha ya Jadon akiwa peke yake kitandani.
"Hata niliwauliza mbona walipanga upya chumba cha kulala kwa sababu haikuwa imeniingia akilini kwamba ningehitaji kitanda cha ziada," Bi McDonald aliandika.
Alisema wasichana hao ni kama wamezaliwa upya.
Wavulana hao walizaliwa wakiwa na mishipa ya damu na sehemu za ubongo zilizoshikana, tatizo ambalo hutokea katika kisa kimoja kati ya visa 10 milioni vya kuzaliwa kwa watoto.
Familia ya McDonald ilikuwa imechangisha $100,000 kugharimia upasuaji huo.
Dkt James Goodrich, aliyekuwa amefanya upasuaji sawa kwa watoto wengine wakiwepo pacha kutoka Syria mapema mwaka huu alijiandaa kwa upasuaji huo kwa kutumia mfano wa 3D.\
BBC
0 comments:
Post a Comment